KAMATI YA KITAIFA YA URATIBU WA UTEKELEZAJI WA USAJILI WA MATUKIO MUHIMU KWA MWANADAMU YAKUTANA OFISI ZA RITA.
===================================================
Wajumbe wa Kamati ya Uratibu wa Usajili wa Matukio Muhimu kwa Mwanandamu (CRVS) ambayo ni  Vizazi, Vifo na sababu zake, Ndoa na Talaka imekutana hii leo jijini Dar es Salaam ili kufanya tathmini ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za KAMATI. Kikao hicho cha siku moja  kimefanyika katika Ukumbi wa mikutano wa RITA Makao Makuu na Kuhudhuriwa na Wajumbe  kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali.