Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Masenza akitoa maagizo hii leo  katika Ufunguzi wa Mafunzo ya siku moja yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa VETA lengo ni kuwajengea  uwezo  Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wake kuhusu kusimamia kikamilifu  Mpango mpya wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa bila ya malipo  Kwa watoto wenye Umri chini ya miaka mitano ambapo  utekelezaji wake utaanza  hivi karibuni katika Mikoa ya Iringa na Njombe, kulia kwake ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bi Emmy Hudson, anayemfuatia kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela na Mwingine ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw Nuhu Mwasumilwe.